Upokonyaji wa Ardhi (Swahili)
Jamii asili dunia nzima wanaona ardhi zao zikitishiwa na sekta za madini, viwanda na kilimo na pia miradi ya maendeleo na kuhifadhi utalii. Filamu hizi zinatazama viwango vya vitisho, wanaoongoza kufanya vitisho hivyo na pia athari za uporaji wa ardhi ulimwenguni. Katika filamu hizi tunasikia taarifa kutoka wanajamii bara la Asia, America ya kusini na Africa ambao ndio wa kwanza kupata dhoruba la athari za unyakuzi wa himaya zao. Kwa nini kufanyika maonyesho ya ‘Upokonyaji wa Ardhi’? Filamu hizi zinafaa kuonyeshwa katika jamii ambazo mashamba makubwa,madini na maendeleo mengine makubwa makubwa yanafanyika ama yanaweza fanyika baadaye. Yaweza pia kufanyiwa maonyesho kwa maafisaa wa serikali, katika vyuo vikuu na umma kwa ujumla ili kuwapa mwamko kuhusu unyakuzi wa ardhi. Dakika kumi na nne 14