Swahili version - Himaya za Maisha

Himaya za Maisha - Mfululizo wa filamu za watu wa Asili

Himaya za Maisha ni Nini?

Vifurushi vya Himaya ya Maisha vinatolewa kutumika bure kwa maelfu ya jamii tofauti duniani kote ambako himaya yao zinaongozwa kwa mtindo wa maisha yao ya kijamii.

Himaya za Maisha ni ya Kina Nani?

Vifaa vya Himaya ya Maisha vinashirikishwa bure kwa maelfu ya jamii tofauti tofauti dunia nzima ambao himaya zao ni muhimu katika maisha yao.

Himaya za Maisha ni ya:

  • Jamii zinazokabili Miradi mikubwa ya kimaendeleo;
  • Jamii ambazo tayari zimekwishapoteza baadhi ama maeneo yao yote na jamii ambazo zimemilikishwa hati miliki ZA himaya zao.
  • Filamu hizi pia ni nyenzo za kujenga uwezo wa mwashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika mengine ya kijamii.
  • Filamu hizi pia zinaweza kuonyeshwa kwa maafisa wa serikali na watu wengine ambao wanahusika au wanaweza kuathiri watu asili na misitu, pia mashuleni, vyuo vikuu na sehemu nyingine za matukio ya uma.

Download - Himaya za Maisha - Kijitabu kwa Mwezeshaji

Upokonyaji wa Ardhi - Je, unyakuzi wa mashamba ni nini? Ni kwa nini unyakuzi huu unafanyika na ina madahra gani?

Mbinu za Kampuni - Filamu hii inaelezea mbinu ambazo makampuni yanatumia ili kuwashawishi wanajamii kuwakubalia na kuwaunga mkono katika miradi yao. Na pia inaonyesha kuwa mbinu hizi zinatumika katika sekta mbalimbali duniani kote.

Umuhimu wa Himaya - Ni nini faida ya umiliki salama wa ardhi kwa jamii asilia, kwa mazingira na kwa jamii kwa jumla?

Haki za Ardhi - Filamu hii inaelezea na kulinganisha mikataba ya jamii katika ardhi ya umma, ardhi za kibinafsi na umiliki wa maeneo ya kijumuiya. Ilamu hii ni maalumu kwa jamii ambazo haki za ardhi bado hazijatambulika, kuwasaidia kujua ni haki gani wanazihitaji.

Mpango wa Maisha - Jamii asilia ya Misak kutoka Colombia wametengeneza na wanatekeleza mpamgo unaoitwa "Mpango wa Maisha", huu ni mpango wa muda unaongozwa na jamii wenyewe katika kuendeleza mipaka yao. Video hii inaelezea maana ya mpango wa maisha, umuhimu wake na hatua muhimu zinazofuaywa katika kutengeneza mkakati wneyewe.

Wanawake mashujaa wa Ololosokwan - Ni hadithi ya harakati nzito ya kudai haki za ardhi na ya kijasiri iliyoongozwa na wanawake wa jamii ya asili tanzania. Mikakati gani walitumia, Changamoto na mafunzo gani waliyaona? Na wanaume wajliipokeaje suala la wanawake kuongoza harakati katika jamii zao?

Hekari nusu Milioni za Matumaini - Kaskazini Mahariki ya Guatemala, miongoni mwa uharibifu wa kale wa Maya na  misitu ya mvua, kuna msitu mkubwa dunia nzima uliotunzwa na jamii. filamu hii inaeneza habari njema na hadidhi kuhusu jinsi gani jamii asilia na jamii kwa ujumla wanavyoshirikiana kuulinda na kudumisha msitu wenye hekari nusu milioni. hili limeta faida za imaisha na watu walio mashinani.                                                                                                           

Mawasiliano - Filamu hii inaangalia jinsi jamii tatu kutoka Indonesia, Tanzania na Ecuador wanavyotiumia redio, mtandao, kuhusisha vyombo vya habari vya kitaifa na vya kimataifa, na pia kutumia Filamu vya mapambano yao ili kuelezea mapambano yao mashinani na duniani kote.

Utumiaji wa Sheria - Jifunze kutoka kwa jamii waliotumia sheria za kimataifa na zile za kitaifa katika kupigania haki zao.

Himaya za Maisha : Utangulizi

Meneo ya maisha ni nini? Filamu hizi ni kwa ajili ya nani? jamii inaweza vipi kutumia filamu katika vifaa vya kifurushi hiki? Dakika kumi na nne 4

Kama mwelekezaji, inafaa kutazama filamu fupi ya utangulizi kabla ya kuangalia filamu nyingine zozote katika mfululizo wa filamu hizi za himaya ya maisha. Itakusaidia kukielewa kifurushi hiki saidizi na kuamua ni filamu ipi katika zilizopo ni muhimu katika jamii.

Download Utangulizi

Upokonyaji wa Ardhi

Jamii asili dunia nzima wanaona ardhi zao zikitishiwa na sekta za madini, viwanda na kilimo na pia miradi ya maendeleo na kuhifadhi utalii. Filamu hizi zinatazama viwango vya vitisho, wanaoongoza kufanya vitisho hivyo na pia athari za uporaji wa ardhi ulimwenguni. Katika filamu hizi tunasikia taarifa kutoka wanajamii bara la Asia,  America ya kusini na Africa ambao ndio wa kwanza kupata dhoruba la athari za unyakuzi wa himaya zao. Dakika kumi na nne 14

Filamu hizi zinafaa kuonyeshwa katika jamii ambazo mashamba makubwa,madini na maendeleo mengine makubwa makubwa yanafanyika ama yanaweza fanyika baadaye. Yaweza pia kufanyiwa maonyesho kwa maafisaa wa serikali, katika vyuo vikuu na umma kwa ujumla ili kuwapa mwamko kuhusu unyakuzi wa ardhi.

Download Upokonyaji wa Ardhi

Mbinu za Kampuni

Filamu hii inaelezea mbinu ambazo makampuni yanatumia ili kuwashawishi wanajamii kuwakubalia na kuwaunga mkono katika miradi yao. Na pia inaonyesha kuwa mbinu hizi zinatumika katika sekta mbalimbali duniani kote. Dakika kumi na nne 14

Wakati jamii zinapofahamu kuhusu mbinu hizi na kujitayarisha kukabiliana nazo. Wanajamii wanaweza kujipanga kwenye nafasi zao na kushikilia maamuzi yanayohusu ardhi kuhusishwa na maendeleo ya nje.

Download Mbinu za Kampuni

Umuhimu wa Himaya

Ni nini faida au umuhimu wa hati-miliki ya ardhi kwa jamii asili? umiliki huu una umuhimu  gani kwa mazingira na nchi kwa ujuma? Dakika kumi na nne 9

Filamu hii inaweza kuonyeshwa kwa jamii, maafisa wa serikali na umma kwa ujumla. Hii yote ni kwa madhumuni ya kueneza ujumbe kuhusu umuhimu wa umiliki rasmi wa ardhi kwa jamii asilia, mazingira na jamii kwa ujumla.

Download Umuhimu wa Himaya

Haki za Ardhi

Filamu hii inaelezea na kulinganisha mikataba ya jamii katika ardhi ya umma, ardhi za kibinafsi na umiliki wa maeneo ya kijumuiya. Ilamu hii ni maalumu kwa jamii ambazo haki za ardhi bado hazijatambulika, kuwasaidia kujua ni haki gani wanazihitaji. Dakika kumi na nne 14

Download Haki za Ardhi

Mpango wa Maisha

Misak ni jamii asilia ambao himaya yao inapatikana Cauca, Colombia.Kama jamii asili nyingi za Latin Amerika, Misak walipoteza himaya zao nyingi katika siku za ukoloni. Katika miaka ya 1970 walianza mchakato wa kurudisha mashamba yao  na walifanikiwa kupata kwa urasmi haki ya ardhi zao kutoka kwa serikali . Tangu wakati huo jamii ya Misak waliendeleza Mpango wa Maisha kama kifaa cha kuamua maendeleo kuhakikisha faida zao zitahifadhiwa kwa vizazi vijavyo. Dakika kumi na nne 23

Download Mpango wa Maisha

Wanawake mashujaa wa Ololosokwan

Filamu hii ni kuhusu wanawake wenye nguvu walio ongoza harakati za haki ya ardhi kwa watu asilia. Bila indini ya wanajamii, sehemu kubwa ya ardhi ya wanajamii hao ilichukuliwa. Pindi wanawake katika jamii hiyo walipogundua kuwa jitihada za kulinda ardhi yao ilishindikana, waliamua kuchukua maamuzi mikononi mwao. Wanawake hao walitumia muamko wa kusimama, kuandamana na shinikizo la kisiasa ili kuongoza  harakati katika kulinda maeneo yao. Dakika kumi na nne 15

Download Wanawake mashujaa wa Ololosokwan

Hekari nusu Milioni za Matumaini

Kaskazini Mahariki ya Guatemala, miongoni mwa uharibifu wa kale wa Maya na  misitu ya mvua, kuna msitu mkubwa dunia nzima uliotunzwa na jamii. filamu hii inaeneza habari njema na hadidhi kuhusu jinsi gani jamii asilia na jamii kwa ujumla wanavyoshirikiana kuulinda na kudumisha msitu wenye hekari nusu milioni. hili limeta faida za imaisha na watu walio mashinani. Dakika kumi na nne 12

Download Hekari nusu Milioni za Matumaini

Mawasiliano

Filamu hii inaangalia jinsi jamii tatu kutoka Indonesia, Tanzania na Ecuador wanavyotiumia redio, mtandao, kuhusisha vyombo vya habari vya kitaifa na vya kimataifa, na pia kutumia Filamu vya mapambano yao ili kuelezea mapambano yao mashinani na duniani kote. Dakika kumi na nne 12

Download Mawasiliano

Utumiaji wa Sheria

Filamu hii inaangalia kesi tatu za kisheria katika mataifa ya  Indonesia, Tanzania na Paraguay ikitumia sheria za kitaifa na kimataifa.  Pia inaangazia faida na  hasara za kuenda kotini. Dakika kumi na nne 13

Download Utumiaji wa Sheria

Ili kupata nakala ya "Himaya za Maisha" bila malipo, tafadahli wasiliana na tuvuti hii info@lifemosaic.net

Jiunge na orodha yetu ya barua pepe


© 2024 Copyright LifeMosaic
LifeMosaic is a Not for Profit Company Limited by Guarantee (Registered company number: SC300597) and a Charity Registered in Scotland (Scottish Charity number: SC040573)